• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 10 September 2017

    waumini wachangia damu baada ya sala ya ijumaa Zanzibar


    Ofisa wa Benki ya Damu Zanzibar Subira Mohammed (kulia), akimpima presha mmoja wa wananchi waliojitokeza kuchangia damu kwa hiyari wakati maofisa wa benki hiyo walipokuwa wakihamasisha uchangiaji baada ya sala ya Ijumaa kwa waumini wa Masjid Sunna Rahaleo mjini Zanzibar Septemba 8, 2017.



    Katika kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiyari, Ijumaa ya Septemba 8, 2017, wafanyakazi wa Benki ya Damu Zanzibar walikuwepo Masjid Sunna Rahaleo mjini Zanzibar kuwashajiisha waumini kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye mahitaji hospitalini. Pichani mfanyakazi Ali Nyanga akimtoa damu mmoja wa vijana waliohamasika.

    Ofisa Uhamasishaji katika Benki ya Damu Zanzibar Bakari Magarawa, akimtoa damu mmoja wa wananchi kwa ajili ya kuipima ili kujua wingi alionao, wakati benki hiyo ilipoendesha uchangiaji wa hiyari Masjid Sunna Rahaleo baada ya sala ya Ijumaa Septemba 8, 2017.


    Ofisa Uhamasishaji wa uchangiaji damu kwa hiyari Bakari Magarawa, akichukua kipimo cha presha kwa mmoja wa waumini wa Masjid Sunna Rahaleo aliyejitokeza kuchangia damu katika kampeni inayoendeshwa na benki hiyo katika misikiti mbalimbali kisiwani Zanzibar

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI