• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 28 October 2017

    ACT – Wazalendo watoa ushahidi kuhusu hali ya uchumi


    Habari

    ACT – Wazalendo watoa ushahidi kuhusu hali ya uchumi

    By  | 



    Chama cha ACT – Wazalendo kupitia Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama hicho, Mh.Zitto Kabwe kimesema kuwa kimetumia takwimu zilizotolewa na BOT kuonyesha kuwa miaka 4 mfulizo mwaka 2014 – 2016, takwimu za ukuaji wa GDP kwa robo ya pili (Aprili – Juni) ya kila mwaka zimekuwa zikishabihiana na nadharia ya uchumi.

    Zitto ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema hali ya takwimu hizo imekuwa tofauti mno kwa robo ya pili ya mwaka 2017, utofauti ambao ndio msingi ulioibua shaka na kusababisha utafiti walioufanya.
    Tutatumia takwimu zinazotolewa na BoT kuonyesha kuwa, kwa miaka minne mfululizo (2014 – 2016), takwimu za ukuaji wa GDP kwa robo ya pili (Aprili – Juni) ya kila mwaka zimekuwa zikishabihiana na nadharia ya uchumi. Hali hiyo imekuwa tofauti mno kwa robo ya pili ya mwaka 2017, utofauti ambao ndio msingi ulioibua shaka na kusababisha utafiti huu. Takwimu zifuatazo zinachambua hali hiyo:
    1. Kwa robo ya pili ya Mwaka 2013 (mwaka unaoishia Juni, 2013), Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilionyesha kuwa Kasi ya Ukuaji wa GDP (y) ilikua kwa asilimia 7. Katika kipindi hicho Kasi ya mfumuko wa bei (p) ilikuwa asilimia 8.5 na kasi ya ukuaji wa ujazo wa fedha (m) ilikuwa asilimia 15.6%. Ukikokotoa (y=m-p) utaona kuwa tofauti kati ya kilichoripotiwa na Benki Kuu na kinachotokana na nadharia ni 0.1 tu, ambayo ndio mzunguko (velocity) wa ujazo wa Fedha katika kipindi husika.
    2. Kwa Mwaka 2014, ilikuwa asilimia 8.6, p ilikuwa asilimia 6.4 na ilikuwa asilimia 15.8. Ukikokotoa (y=m-p) utaona tofauti ya y ya nadharia na iliyoripotiwa na BOT ilikuwa asilimia 0.8, ambayo ndio mzunguko (velocity) wa ujazi wa fedha katika kipindi husika.
    3. Mwaka 2015, y ilikuwa asilimia 5.7, p ilikuwa asilimia 5.9 na m ilikuwa asilimia 13.1. Ukikokotoa (y=m-p) zinakupa tofauti ya y ya BoT na ya nadharia kuwa asilimia 1.5, ambayo ndio mzunguko (velocity) wa ujazo wa fedha katika kipind
    4. Mwaka 2016, y ilikuwa asilimia 6.8, p ikawa asilimia 5.3 na m ilikuwa asilimia 12.6. Ukikokotoa (y=m-p), hii inakupa tofauti ya asilimia 0.5 kati ya nadharia nakilichoripotiwa na Benki Kuu. Hizi zote ni takwimu zinazotolewa na Benki Kuu na tofauti inaweza kukokotolewa na mtu yeyote anayejua kuhesabu.
    5. Sasa tuangalie kilichoripotiwa kwa robo ya pili ya mwaka 2017. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa takwimu za ukuaji wa GDP kwa robo inayoishia Juni 2017.
    Taarifa hiyo inaonyesha kuwa Pato la Taifa lilikuwa kwa kasi ya asilimia 5.7 na mfumuko wa bei asilimia sita wakati ujazo wa fedha (M3) ulikua kwa kasi ya asilimia 6.1. Kasi ya ukuaji wa ujazi wa fedha inathibitisha kelele za miezi mingi kuhusu mzunguko wa fedha kuwa mdogo hivi karibuni. Utaona kuwa m ya M3 imeshuka kwa takribani asilimia 51.5 kutoka 12.6 ya robo ya pili ya mwaka 2016 mpaka 6.1 kwa robo ya pili ya mwaka 2017. Ukichambua takwimu hizi Kwa kutumia nadharia (y = m-p) utaona kuwa Tanzania ilikuwa na msinyao wa uchumi kwenye robo husika .

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI