• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 31 October 2017

    Benki ya Biashara ya PTA yabadili jina

    Benki ya biashara na maendeleo mashariki na kusini mwa afrika maalufu kama TPA imebadili rasmi jina la biashara Leo na kuanza kutumia jina la TDB
    Hayo yamesemwa Leo na Afisa mkuu mtendaji wa benki hiyo bw.Admassu Tadesse alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuwa benki hiyo kuanzia 31 October itakuwa ikitumia jina la  benki ya biashara na maendeleo(Trade and Development Bank)yaani TDB ikiambatana na nembo mpya ya jina hilo.
    Aidha Tadesse amesema jina la usajili kisheria  la benki ya biashara na maendeleo mashariki na kusini litabaki pale pale kama lilivyo na kuongeza kuwa itaendelea kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye sekta zenye kupewa kipaumbele kama vile miundo mbinu,viwanda na biashara ya kilimo miongoni mwa nchi 21 inamofanyia shughuli zake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
    Hata hivyo Tadesse amesema usanifu wa jina letu unaashiria kuwa tumeibuks na nguvu mpya na dhamira mpya katika kuimarisha biashara,maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kikanda katika kipindi ambacho ukanda mzima umeinua kwa dhati kusukuma mbele mageuzi ya kiuchumi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
    Vile vile bw.Tadesse amemaliza kwa kusema  kubadili jina kumekuja baada ya miaka kadhaa  ambapo ubora wa Mali umeongezeka ,upatikanaji faida umepanda na ubunifu unatumika ipasavyo hivo vitu vilivyotokana na mageuzi kadhaa na muundo mzima wa benki yanayolenga kuimarisha na kuifanya iwe kisasa zaidi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI