• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 13 October 2017

    Jenista Muhagama akabidhiwa mwenge na Mkuu wa mkoa Mjini Magharibi Unguja

    Baada ya mwenge wa uhuru kuanzia mkoani Katavi, hatimaye leo Oktoba 14,
    umewasili na unatarajia kuzimwa katika uwanja wa Taifa wa Aman, kisiwani
    Zanzibar katika mkoa wa Mjini Magharibi , ambapo mkuu wa mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud , ameukabidhi mwenge kwa serikali na umepokelewa na waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, Kazi, Vijana, ajira na walemavu, Jenista Mhagama .
    Baada ya makabidhiano hayo hafla hiyo itahamia katika kanisa la romani katoliki kwa ajili ya ibada maalum ya kumuombea na kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa,
    Mwl Julius Nyerere , ibada hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John
    Magufuli, Makamu wake Samia Suluhu Hassan , Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi wengine waandamizi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI