Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) Limetangaza maandamano nchi nzima ya kudai katiba mpya.
Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam
wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa
(JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya ya mkutano Mkuu wa Jukwaa
hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia
kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.
“Tumeazimia kufanya maandamano siku ya tarehe 30 ya
mwezi huu, katika ngazi ya kitaifa ambayo yatafanyika Jijini Dar es
Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA hapa Mwenge Saa nne asabuhi na
yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja” amesema Mwakagenda.
Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari
limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam
kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo
“Maandamano haya ni ya amani ili kurudisha hamasa ya
wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia hapa
nchini”
“Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia
tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya
amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja” Amongeza Kusema Mwakagenda.
No comments:
Post a Comment