• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 29 October 2017

    Kijana amtwanga risasi mke wake kisa hela ya matumizi

    Polisi wilayani Babati mkoani Manyara inamshikilia, Cosmas James kwa tuhuma za kumuua mzazi mwenzie, Regina Daniel (23) kwa kumpiga risasi.
    Cosmas ambaye ni askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wilayani Babati, alifuatwa na mkewe akiwa lindoni na kuombwa pesa ya matumizi ndipo mzozo wa wawili hao ulipoanzia kisha mwanaume huyo kumfyatulia risasi mke wake.
    Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema kuwa tukio hilo limetokea mjini Babati jana saa 12:30 jioni, ambapo bwana Cosmas alikuwa lindoni katika Benki ya NMB tawi la Babati.
    Kamanda Tibishubwamu amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kabla ya kifo cha mwanamke huyo, kulitokea mzozo kati ya wawili hao kuhusu fedha za matumizi ya mtoto .
    Wakati wakiendelea na mzozo, ndipo askari huyo kwa kutumia silaha aliyokuwa nayo alimpiga Regina risasi nne kwenye paji la uso, kifuani na shingoni,” amesema Kamanda Tibishubwamu .
    Kamanda Tibishubwamu ameongeza kwa kusema kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa aliitelekeza silaha lindoni na kwenda kujisalimisha polisi .
    Mtuhumiwa yupo mahabusu kwa mahojiano kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa Babati ya Mrara.
    Chanzo:Mwananchi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI