Arusha. Madiwani watatu wa Chadema waliojiuzulu katika Halmashauri ya
Meru mkoani Arusha na kujiunga na CCM, wameangushwa katika kura ya maoni
ndani ya chama hicho.
Madiwani hao waliojiuzulu hivi karibuni kwa kile walichoeleza ni
kutokana na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli waliomba kutetea
nafasi zao.
Waliogombea na kuangushwa ni Solomon Laizer, aliyekuwa diwani wa
Ngabobo, Japhet Jackson (Embuleni) na Anderson Sikawa (Leguruki).
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meru, Andrew Mungure amesema leo Jumatano
Oktoba 18 kuwa, matokeo ya kura ya maoni si mwisho wa uteuzi. Uchaguzi
huo ulifanyika jana Jumanne.
Mungure amesema wagombea katika kata hizo watajulikana baada ya vikao ambavyo vimeanza leo.
"Leo wanajadiliwa wagombea wote ngazi ya kata, baadaye tutajadili kamati
ya siasa na halmashauri kuu ya mkoa ndipo watapitishwa wagombea,"
amesema.
Amesema kutokana na mchakato huo, matokeo ya kura ya maoni si mwisho.
Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Aloyce Hayuma amekiri madiwani hao kugombea na kushindwa. Hata hivyo, amesema mchakato unaendelea
No comments:
Post a Comment