• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 1 October 2017

    Meya wa jiji la Dar Mwita ashauri Taasisi za kibenki kuwapatia walemavu wasioona mikopo.

    MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezishauri Taasisi za kibenki kuwasaidia watu wenye ulemavu wasioona ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali ili waweze kujitegemea wenyewe.

    Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa jana wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya wanawake wenye ulemavu wakusikia (Viziwi) (FUWAVITA) yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini hapa.

    Meya Mwita alisema kuwa walemavu wananafasi kubwa ndani ya jamii kutokana na ushiriki wao katika shughuli za kimaendeleo na kwamba wanapaswa kupewa fursa zamikopo na Taasisi za kibenki ili waweze kujiondoa kwenye changamoto za kimaisha.

    " Ulemavu sio ugonjwa, kuwa mlemavu haimaanishi kwamba ndio wasisaidiwe, makundi kama haya ambayo yameonyesha nia ya kujitafutia weyewe , wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja " alisema Meya Mwita.

    " Makundi haya yamesahaulika katika jamii yetu, ni muda wetu huu kuwakumbuka, vyombo vya habari pia vitumike kutangaza bidhaa ambazo zinazalishwa na makundi haya, wananchi nao wajitokeze kuunga mkono jitihada zao" aliongeza .

    Awali akijibu risala iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa FUWAVITA  Anethi Jerana ,Meya Mwita alisema kuwa jiji litawapatia mkopo wa shilingili milioni tatu kama walivyoomba na kuwakaribisha kuomba tena iwapo watahitaji.

    Katika hatua nyingine Meya Mwita aliipongeza Benki ya NMB kwakudhamini maonyesho hayo sambamba na kutoa huduma ya kuwafungulia akaunti za kifedha na kutumia nafasi hiyo kuzishauri Benki nyingine kuiga mfano huo.
    Mapema mwenyekiti wa FUWAVITA akisoma risala mbele ya Mstahiki Meya Mwita aliomba Halmashauri ya Jiji iwasaidie mkopo wa shilingi milioni tatu , ili waweze kuendeleza shuguli zao za kuzalisha bidhaa mbalimbali kwenye kikundi chao.

    Mbali na mkopo huo, pia waliiomba Halmashauri ya Jiji kuwapatia vyumba vilivyopo kwenye viwanda vidogo  Mwananyamala ambavyo vilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI