……………………………………………………………
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo
na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji
mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.
Katika maeneo aliyopita ameweza
kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja,
na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili
ya matumizi.
Naibu Waziri Aweso alisema ipo
haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa
ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa
changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.
“Nitakaa na taasisi za DAWASA na
DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha
kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya
wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya
kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.
No comments:
Post a Comment