
Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo leo wakati akizungumza na wakazi wa kata za Mgagao na Kirya zilizopo wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Amesema Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo makini na kuhakikisha usalama wananchi wa eneo.
Amesema Serikali ipo makini na ina macho na masikio ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.
"Jambo limeshapita acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua kwamba Serikali ina mkono mrefu atakayethubutu kutenda mambo ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.
Ulega amedai kupata taarifa za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao vya kumtafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo
Mbali na hilo, naibu waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali ya Rais John Magufuli ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge na kwamba, haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.
No comments:
Post a Comment