Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Ndug Humphrey Polepole leo tarehe 07 Oktoba, 2017 amehudhuria katika
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Wanging’ombe
Mkoani Njombe akimuwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Ndugu Philipo Mangula.
Mkoani Njombe akimuwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Ndugu Philipo Mangula.
Mkutano Mkuu huo wa Wilaya ukiwa
ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali za ndani ya Chama zinazoendelea
Nchini kote ulihudhuriwa na jumla ya wajumbe 718 kutoka kata zote
Ishirini na moja za Wilaya ya Wanging’ombe.
Katika Mkutano huo Ndg.Polepole
aliwapongeza wanachama na Viongozi wote wa Chama Wilaya ya Wanging’ombe
kwa kazi kubwa ya Ushindi wa asilimia mia moja katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 na kushinda viti vyote vya Vitongoji, Vijiji Udiwani, Ubunge,
na kura nyingi walizompatia Rais.
Mbali na hilo Ndg Polepole
aliwasisitiza wajumbe wa Mkutano Mkuu kuchagua viongozi waadilifu,
wachapa kazi, wanaochukizwa na Rushwa, wanaopenda watu zaidi kuliko
wanavyojipenda wao na yote kwa yote wanaokisi utendaji kazi wa Rais na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu John Pombe Joseph Magufuli ili
kuendana na kasi ya CCM Mpya ambayo ndio chachu ya Tanzania Mpya.
Ndg. Polepole aliendelea kwa
kueleza juu ya kazi moja kubwa ya Chama Cha Mapinduzi kwa kumnukuu Mwl.
Nyerere”Kazi kubwa ya Chama Cha siasa ni kuwasemea watu na kua kama
daraja kati ya watu na serikali inayowaongoza”, Hivyo Viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi(CCM) ni lazima muwasemee watu popote mlipo ili hata wasio
wanaCCM waone na waendelee kuamini ninyi ni watu sahihi.
Zaidi Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi alieleza juu ya umadhubuti wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) kikiwa ni
Chama bora kwa Itikadi, Muundo, Utendaji, Idadi kubwa ya Wanachama hai
mpaka sasa kina jumla ya wanachama wanaokadiriwa Milioni 14, kwa
Afrika kikifuatiwa na ANC cha Afrika ya Kusini na kikishika nafasi ya
Pili Duniani kikiongozwa na Cha cha Kikomunisti cha watu wa Uchina.
Hivyo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ni lazima mtembee kifua mbele
Afrika na Dunia kwa ujumla kua tupo kwenye Chama sahihi na madhubuti
chenye kujali Demokrasia kuanzaia ngazi ya Mashina.
Ndg. Polepole alimalizia kwa
kueleza dhamira njema ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Ndg.
Magufuli katika kupambana na wala rushwa, wahujumu uchumi, mafisadi na
akiweka msisitizo kwamba wote watakaobainika kushiriki uchakachuaji wa
pembejeo za wakulima CCM imeelekeza Serikali kuwachukulia hatua kali za
kisheria.
Uchaguzi wa leo Wilaya ya
Wanging’ombe ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali zinazoendelea Nchi
nzima zikianza ngazi ya Mashina na sasa ni Ngazi za Wilaya.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
No comments:
Post a Comment