• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 1 October 2017

    Siku ya Wazee Duniani: DC Mjema agawa vitambulisho kwa wazee


    Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo ameowaongoza wanailala kusherekea siku ya Wazee Duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo ameagawa vitambulisho vya wazee kwa ajili kupata matibabu bure ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli imedhamiria kuwaenzi na kuwapatia  huduma bora wazeee kutokana na mchango wao katika taifa.

    " Wazee hawa ni hazina katika taifa letu wanahitaji kuenziwa matunda ya leo katika taifa leo ni kutokana na mchango wao, hivyo serikali ya awamu ya tano haitowaacha nyuma itandelea kushirikiana nao" Alisema DC Mjema.


    Katika kuboresha huduma za wazee DC Mjema amepiga marufuku  wazee kutozwa huduma za choo kwenye vyoo vya umma, huku akihaidi kushughulikia suala lao la kutolipa nauli kwenye magari ya mwendo kasi na tozo ya kiingilio kituo cha mabasi cha Ubungo, ambapo amehaidi kuongea na mamlaka husika ili wazee hao waweze kupata huduma hizo bure.


    " Haya masuala yapo ndani ya uwezo wetu tutazungumza na mamalaka husika kuangaalia ni jinsi gani tunawasaidia wazee hawa kama walivyoeleza kwenye risala yao" Alisema DC Mjema.


    Pia DC Mjema amewaomba wazee kuwa chachu ya maadili mema kwa kuendelea kuihusia jamii ili vivazi vinavyokuja viendelee kuwa na nidhamu  na utii kwa jamii inayowazunguka.


    Kuhusu suala la kutolipia huduma za maji kwa wazee DC Mjema ameeleza kuwa suala hilo linawezekena ila kwa wazee watakao kuwa wanamiliki nyumba zao na siyo nyumba za kupanga, pia DC Mjema ameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutenga fungu maalum kwa ajili ya wazee ili waweze kujikwamua kiuchumi.



    Katika hatua nyingine DC Mjema amekabidhi kati za matibabu kwa wazee 500 kwa siku ya leo huku jumla ya wazee 15000 wakitaraji kupatiwa vitambulisho hivyo vitakavyo wawezesha kupata matibabu ndani na nje ya wilaya ya Ilala.


    Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya ilala Dr Victorina Ludovick amesema wilaya ya Ilala inaidadi ya wazee wapatao 42,000 na zoezi la kuwapatia kadi wazee wote litakamilika mwezi June 2018.


    Kwa upande wake Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ameeleza kuwa licha ya milioni 200 zilizotengwa halmashauri inampango wa kuongeza kiwango hicho ili kuwawezesha wazee.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI