Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo
Amesema
Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ni inawajali watu wanyonge hivyo wafugaji hao wavulimie na kwamba timu iliyoundwa na waziri mkuu siku za nyuma ikiwa baadhi ya viongozi wao wakiwemo madiwani.
“Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba msiharibu hali ya hewa hii ndiyo rai yetu.Au kuna yeyote anayepinga jambo hili? Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.
“Hatua hii itaturahisishia sisi kwa sababu wizara inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana sehemu kubwa ya nchi wafugaji wamekuwa na malalamiko makubwa sana ikiwemo kufilisiwa mifugo yao pindi inapoingia hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto inayowakabili wafugaji hao kutokana na maeneo machache yaliyopo.

Hata hivyo, Ulega alihaidi kushughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni kwa wafugaji hao.
No comments:
Post a Comment