• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 22 November 2017

    Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi Mugabe ataapishwa Ijumaa

    Emmerson Mnangagwa
    Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa, limesema shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC)
    Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.
    Robert Mugabe
    Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.
    Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.
    Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:Raia wa Zimbabwe wakisherekea kujiuzulu kwa MugabeRais wa Zimbabwe walishangilia kujiuzulu kwa Mugabe mjini HarareBaadhi ya rais walipeperusha bendera ya ZimbabweAsakari wa Zimbabwe pia walisherehekea kujiuzulu kwa Bwana Mugabe
    Katika barua hiyo , Bwana Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu ukabidhianaji wa mamlaka wa amani, na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
    Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI