Harusi ya mwanaume mmoja jijini Blantyre, nchini Malawi imeingia doa
siku ya jumamosi ya wikiendi iliyopita baada ya mwanamke mmoja kusimama
mbele ya kanisa na kudai kuwa bwana harusi ni mchumba wake na alimuahidi
kumuoa.
Kwa mujubu wa maelezo kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa
limetokea katika kanisa la Living Waters Church (LWC), Dayosisi ya
Chilimba mjini Blantyre. Ambapo waumini wamesema walishtuka ghafla
kumuona mwanamke huyo aliyekuwa amevalia suti akikimbia mbele ya altare
baada ya Mchungaji kutangaza kuwa kama kuna mtu anapingamizi ajitokeze
kanisani hapo.
Tukio hilo lilianza kusambaa kwenye mtandao wa Twitter baada ya mdau
mmoja kurusha picha hizo mtandaoni kabla ya kunaswa na vyombo vya
habari.
Hata hivyo baada ya tukio hilo kutokea Mchungaji alilazimika
kusimamisha zoezi hilo kwa muda lakini baadae Bi. Harusi alirejea na
shughuli kuendelea. Ingawaje haijatolewa taarifa rasmi kuhusu mahusiano
kati ya Bwana Harusi mwanamke huyo aliyejitokeza kanisani hapo.
..
Monday, 6 November 2017
Habari
No comments:
Post a Comment