Dar es Salaam – Katika jitihada za
kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya
umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni Marathon, mbio
hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi
Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mkurugenzi wa Events World alisema, Lengo kuu
la “Kigamboni Marathon”
ni kutangaza fursa za
uwekezaji, vivutio vya kitalii na
Biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya
Mhe. Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia
Suluhu Hassan katika kuhamasisha
Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.
Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia
Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya
wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa
‘kigamboni Marathon’ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea
uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.
Nae Mratibu wa Mbio hizo Mr. Juma K.
Mtetwa alisema ni ukweli ulio wazi ya kuwa Kigamboni imezunguukwa na maeneo
mazuri zaidi ya kimichezo, Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote ile Jijini
Dar es saalam na hiyo ni sababu moja wapo inayotupelekea kuamini kuwa ‘Kigamboni
Marathon’ itakuwa ni miongoni mwa mbio bora zaidi Tanzania itakayoibua
wakimbiaji wazuri watakao watakaoleta ushindani mkubwa katika Mchezo huu wa
riadha Duniani kote.
Kigamboni Marathon imepangwa kufanyika
katika viwanja vya mji mwema jirani na ofisi za Halmashauri mpya ya kigamboni
tarehe 2 mwezi wa 12, 2017 ikiwa na Mbio za urefu wa kilomita 21(Half
Marathon), Kilomita 10 na Mbio kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na
mazoezi ya mara kwa mara (Fun Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo
Medali za dhahabu, Silver na Gold pia Pesa Taslimu kwa washindi.
Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya
‘kigamboni Marathon’ natanguliza Shukrani kwa wadau wote waliojitokeza kuunga
mkono katika Jambo hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa letu wakiwemo Viongozi
wetu ndani na nje ya Kigamboni, wanahabari, Taasisi Mbali mbali, Makampuni na
Jamii kwa Ujumla.
Pia alizishukuru kampuni
zilizojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwemo Property International, Itel Mobile,
Coca cola kupitia kinywaji cha Dasani, J.P.M Hospital, Akemi Restaurant, PCMC
Hospital na Red Bull na kuomba wadau na makampumi mbali mbali kujitokeza na ku-
support mbio hizo.
Alisema Ushiriki wa Makampuni makubwa
kutoka ndani na Nje ya Kigamboni unatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni
na kuwasihi wanakigamboni kuitumia fursa hiyo kujumuika pamoja na kuonyesha
walichonacho lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.
Napenda kuchukua fursa hii pia
kuwakaribisha Wadhamini,Washiriki na Wadau mbalimbali katika tukio hili la
Kipekee lenye Usalama na Ustaarabu wa Hali ya juu.
Kwa maelezo juu ya ushiriki tafadhari
wasiliana na: 0784 959 509 / 0753 777 666, email:kigambonimarathon@gmail. com
Njooni tuungane kwa Pamoja na Kuyapa
Thamani Maisha yetu,
No comments:
Post a Comment