Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV.
…………………………………………………………….
Dodoma Mjini
Anthony Mavunde wampongeza Mh. Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli kwa
uamuzi wake kuhamishia Makao makuu ya Serikali Dodoma na hivyo kuongeza
fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kupitia uzalishaji wa bidhaa na
huduma mbalimbali zitakazotolewa.
Wakizungumza leo
katika kipindi cha 360 cha Clouds TV wamesema uamuzi huo ni fursa muhimu
kwa wanadodoma ni vyema wakaitumia ipasavyo.
Aidha wamempongeza
Mh. Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja CDA na kurudisha mamlaka
ya utawala wa ardhi chini ya Manispaa ya Dodoma na kubadilisha mfumo wa
umiliki ardhi kutoka katika upangaji(Lease Ground) kwenda kwenye mfumo
wa hati ya umiliki.
Wamesema kupitia mfumo huo Dodoma itapata fursa ya kuvutia zaidi wawekezaji wa muda mrefu tofauti ilivyokuwa awali.
Aidha Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameelezea mipango mikubwa ya ukuzaji
mji wa Dodoma ikiwemo uharakishwaji wa huduma ya vibali vya
ujenzi,upimaji wa mae uboreshwa wa miundombinu na huduma za kijamii ili
viende sambamba na ukuaji wa haraka wa mji wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment