Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amezindua ujenzi wa ofisi za walimu wa mkoa wa Dar es salaam katika shule ya ma msingi kichangani kwa lengo la kuwaboreshea mazingira mazuri ya kufundishia wanafunzi.
Akizungumza katika uzinduzi huo RC MAKONDA amesema ujenzi wa ofisi hizo utasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili walimu katika utendaji wa kazi zao, hali ambayo inasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa mkoa huo.
Aidha Makonda ameahidi kuwa baada ya kukamilikaa kwa ujenzi huo vifaa vitakavyobaki vitatumika katika kujenga ofisi za shule ya
msingi majohe iliyopo karibu na shule hiyo.
Kwa upande wa Mkuukuu wa wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA amempongeza Rais Magufuli Kwa kazi zake za kimaendeleo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa jitihada zake katika kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili kuweza kutoa elimu bora na ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment