Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga
(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakitwanga Kinu
wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa
(Boma) jana Mkoani humo.
Na Hamza Temba – WMU
………………………… ………………………… ……..
Katika jiihada za Serikali za kuendeleza ushirikiano na jamii
zinazozunguka maeneo ya hifadhi nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii
imetoa msaada wa mabati sitini kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule ya
msingi Kipanga baada ya kuezuliwa na kimbunga hivi karibuni katika
kijiji cha Ubwachana Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Msaada huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga alipotembelea kituo cha Malikale cha Isimila mkoani
humo ambacho kinapakana na shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya
siku moja Mkoani humo.
Akikabidhi mabati hayo, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali inatambua mchango wa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kwenye uhifadhi shirikishi hivyo ni jukumu la Serikali kuwaunga mkono pale wanapopatwa na majanga ya aina mbalimbali.
Aidha, aliwataka baadhi ya wananchi wanaochimba mchanga kwenye maeneo ya vivutio katika kituo hicho waache mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwakuwa wanahatarisha uhai wa kingo za miamba ya kale ambayo na kivutio kikubwa cha utalii wa asili katika ukanda wa kusini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya mambo ya Kale wa Wizara hiyo, Bi. Digna Tillya alitoa rai kwa wananchi wanaozunguka kituo hicho kushirikiana na Serikali katika uhifadhi na ulinzi wa kituo hicho na kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa mazingira.

(kulia) akiwa amevaa “musk’ mfano wa vazi la kabila la wahehe wa Mkoa wa
Iringa wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa
huo (Boma) jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa
tatu kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubwachana, Donatus
Lihoha mabati 60 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vya shule ya
msingi Kipanga ambayo iliezuliwa na kimbunga hivi karibuni ikiwa ni
kutambua mchango wa wananchi katika uhifadhi shirikishi wa Kituo cha
Mali Kale cha Isimila jana Mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili
kushoto) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye
pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na
Uhuishaji, Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini
kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara
yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa,
Richard Kasesela (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo
ya Kale wa Wizara hiyo Digna Tillya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia)
akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni
Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na Uhuishaji,
Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini wakati akitoa
maelezo kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati
wa ziara yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Richard Kasesela (kulia kwake).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia)
akizungumza na watumishi wa Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa
(Boma) alipotembelea Makumbusho hiyo jana wilayani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili
kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela kuhusu
Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara yake
jana Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wapili
kushoto) akisalimiana na wafanyakazi wa (Kituo cha Mali Kale cha
Isimila) alipotembelea kituo hicho jana mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto)
akimpa maelekezo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert
Masunya (kulia) alipotembelea Kituo cha Mali Kale cha Isimila mkoani
Iringa jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Digna Tilya akizungumza wakati wa hafla hiyo ya
kukabidhi mabati.
Baadhi wa washiriki wa hafla hiyo.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment