Serikali imeimizwa kuharakisha mchakato Wa katiba mpya ili haki zipatikane kwa urahisi katika mambo mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na wakili mwanasheria wa haki za binadamu
Bw. Deogratious bwire alipokuwa akizungumza na wadau mbali mbali wa haki
za binadamu katika mkutano Wa tathimini ya mapendekezo ambao
ulifanyika katika ukumbi wa classic Hall ubungo Plaza ambapo wanafanya
tathimini wa mapendekezo 131 ambayo serikali imeyakubali kuyatekeleza
ikiwemo Haki ya kupata taarifa na vyombo vya habari, haki za kijamii,
haki za Watoto, haki za uchumi,haki za watetezi wa haki za kibinadamu na
nyinginezo mbali mbali ambapo amesema kuna ulazima wa kupata katiba
mpya ambayo imelenga vitu mbalimbali vilivyomo kwenye mapendekezo ambayo
serikali imeyakubali kuyafanyia Kazi.
Hata hivyo Bw. Bwire amesema tathimini ya mapendekezo
yanayofanyika yanaumuhimu mkubwa kwani baada ya mapendekezo asasi mbali
mbali na wadau wa haki za binadamu huchukua hatua mbali mbali zenye tija
kwa taifa kwani huipa nguvu tume ya haki za binadamu pamoja na kufanya
utafiti wa kuona bajeti wanayopewa haki za Binadamu na kazi wanazopewa
kufanya ili kuona namna ya kusaidia tume hiyo kwani UPR inafanya Kali
kwa kushirikiana na serikali ambayo ndio watekelezaji Wakuu, sekta
binafsi Hawa huwasaidia maswala ya kifedha pia na tume yenyewe za haki
za binadamu.
No comments:
Post a Comment