Serikali imepiga marufuku utoaji wa fedha kwa wakandarasi ambao
hawajaonyesha tafiti za uhalisia wa eneo wanalokwenda kufanyia kazi ili
kuepuka gharama na hasara na ziada ya fedha zinazoweza kujitokeza wakati
wa utekelezaji wa mradi husika.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mheshimiwa Juma Aweso mara baada ya kukutana na viongozi, wafanyakazi
pamoja na wanafunzi wa chuo cha maji nakusema serikali imejiwekea
mipango mikubwa ya kumaliza tatizo la maji ikiwa ni pamoja na kusimamia
wataalamu wake wanafanya kazi kwa uweledi na kutatua tatizo la maji
ambalo limekua sugu kwa miaka mingi.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt.Shija Kazumba ameiomba serikali kuboresha miundombinu wanayoitumia ili kuendana na kasi ya dunia
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt.Shija Kazumba ameiomba serikali kuboresha miundombinu wanayoitumia ili kuendana na kasi ya dunia
No comments:
Post a Comment