Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dkt.
Faustine Ndugulile leo amefungua kongamano la Kisayansi la Hospitali
ya Taifa Muhimbili na kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kutoa
muongozo mpya wa matumizi ya dawa ili kudhibiti matumizi holela ya
dawa.
Amesema muongozo huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya dawa ambayo yanachangia usugu wa dawa katika mwili wa binadamu.
“Muongozo
huu mpya utakapotolewa utatumika katika Hospitali zote nchini na pia
serikali tayari imeoredhesha dawa muhimu na dawa hizi zinapatika kwani
serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shiling bilioni 30 hadi kufikia
bilioni 269,” amesesisitiza Dkt. Ndugulile.
Pia,
Naibu Waziri Ndugulile ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha
inapunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Muhimbili
tayari imeanza kutoa huduma ya kupandikiza figo, kufanya upasuaji wa
kuwawekea vifaa vya kuwasaidia watoto kusikia na sasa wataalam wengine
wanajiandaa kwenda India ili kujengewa uwezo wa kufanya upasuaji wa
kupandikiza Ini.
“Nimefurahishwa
sana na mipango mikakati mliyojiwekea na kutoa huduma za kibingwa za
juu hapa nchini , baadhi zikiwa za kwanza kwenye sekta ya Umma hata
kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki hasa upandikizaji wa vifaa vya
kusikia na figo,’’ amesema Naibu Waziri.
Awali,
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence
Museru amesema pamoja na changamoto mbalimbali hospitali hiyo
inaendelea kuboresha huduma zake na tayari imeongeza mashine za kuchuja
damu kutoka 17 hadi 42, vyumba vya upasuaji kutoka 13 hadi 20 pamoja na
kuongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka 21 hadi 88.
Kongamano
hilo la Kisayansi ni la kwanza kufanyika MNH ambalo limebeba mada kuu
inayosema changamoto na fursa za utoaji tiba nchini.
Mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo magonjwa ya Figo , Upandikizaji Figo na Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini.
No comments:
Post a Comment