Na Stahmil Mohamed.
Wataalamu wa teknologia ya habari na mawasiliano(TEHAMA)wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na ili kutovunja amani iliyopo nchini.
Wataalamu wa teknologia ya habari na mawasiliano(TEHAMA)wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na ili kutovunja amani iliyopo nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano
Mhandisi Atashita Nditiye alipokuwa akizungumza na wataalamu wa sekta ya
habari na mawasiliano alipotembelea katika kitengo hiko kwa Mara ya
kwanza tangu alipoteuliwa kwenye nafasi hiyo ambapo ameahidi
kushirikiana kikamilifu na sekta hiyo habari na mawasiliano katika mambo
mbalimbali ya kukuza uchumi wa taifa pia kwa kuwadhibiti wataalamu wa
kweli wa sekta ya mawasiliano kuendana na maadili ya kazi pamoja na
sheria zilizopo kikamilifu ili kuepusha migogoro mbalimbali kwakuwa
sekta ya mawasiliano ni kubwa na inategemewa na jamii katika
kuwahabarisha na kuwapa taarifa mbalimbali zinazotokea hivyo kama
maadili ya kazi pamoja sheria hazitafuatwa machafuko yanaweza kutokea.
Aidha Mhandisi Nditiye amedhamiria kuwachukulia hatua Kali
za kisheria kwa wataalamu wa mawasiliano wasiofata maadili ya kazi
pamoja na kuwadhibiti wataalamu feki wa sekta ya mawasiliano kwakuwa hao
ndio wanaoifanya sekta ya mawasiliano kudharauliwa kwa kutokufata
maadili.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa watahakikisha wataalamu wa
sekta ya mawasiliano wanasajiliwa haraka ili watambulike kwa urahisi
kwakuwa ni taaluma tegemezi nchini.
Naye katibu mtendaji wa kitengo cha Teknologia ya
mawasiliano Mhandisi Samson Mwella amesema sekta ya mawasiliano ni
sekta ambayo imekuwa kwa 13% na ni sekta ambayo inamechangia uchumi wa
nchi kwa 2%japo kuwa kunachangamoto mbali mbali zinajitokeza na anaamini
changamoto hizo zikitatuliwa kikamilifu sekta ya mawasiliano inaweza
kuchangia uchumi wa nchi kwa asilimia kubwa zaidi kama ilivyo kwa nchi
nyingine.
Aidha Mhandisi Mwella ameongeza kwa kusema kuwa sekta ya
mawasiliano ni sekta ambayo inatoa ajira za moja kwa moja kwa watu
mbalimbali wanaojishughulisha hivyo anaitaka serikali iwaezeshe
wataalamu wa mawasiliano kwani imegundulika katika bidhaa laki moja
zinazozalishwa katika viwanda bidhaa nne zinatokana na tehama sawa na
0.004%hivyo hakuna budi kutilia mkazo katika sekta hiyo.pia amesema
wataalamu wameamua kuanza kupanua wigo wa kufikisha mawasiliano kwa
lugha ya kiswahili na picha ili iwafikie kwa umma wote kwa urahisi kwa
wasiojua lugha pia kwa watu ambao hawasikii au kuelewa kwa lugha
maandishi.
No comments:
Post a Comment