• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 18 November 2017

    WATUMISHI WA AFYA BADO WANAHITAJIKA NCHINI



    WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuikisha nchi katika uchumi wa viwanda  kufikia 2020.

    Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM  yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

    "Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za  afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89,842 na bado tunahitaji watumishi 95,800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt.Ndugulile.

    Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani kimekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

    Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya  imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

    "Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba was Chuo  hicho Dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza kielimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.

    “Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema Dkt. Musika

    Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Mhitimu wa fani ya Udaktari ngazi ya stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.

    Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika  kada mbalimbali za sekta ya afya.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI