Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka IGP, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa
kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka
kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi
kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.
Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.
“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”
Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Mawakala wa Forodha kuhakikisha wanakuwa makini katika kazi zao na Serikali haitawavumilia wababaishaji kwani inasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment