Mrembo wa Tanzania na Muigizaji Wema Sepetu amemfunga mdomo muigizaji
mwenzake Steve Nyerere kwa kumwambia hana mawazo ya kurudi CCM kama
jinsi ambavyo wengine wanavyofanya.
Steve aliandika "Sasa utakuwa mzalendo wa kweli , Msando naheshimu maamuzi yako maana ni maamuzi sahihi, kwako pamoja na family yako , rafiki zako nasi tupo pamoja nawe, soon na yuleeeeeeeee rafiki yetu , dada yetu , msanii mwenzetu , naye yupo njiani kurudi nyumbani"
Hata hivyo Wema Sepepetu baada ya kuona ujumbe huo ambao alihisi kama inamlenga yeye, alijibu chini ya ujumbe huo kwa kuandika "I hope hauniongelei mimi... Maana mawazo hayo sina"
Muigizaji Wema Sepetu alihama ndani ya chama cha mapinduzi Februari mwaka huu kwa madai kuwa ameamua kujiunga na Chadema kupigania demokrasia ya kweli.
No comments:
Post a Comment