• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 1 November 2017

    Wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa dar es salaam yatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Biafra.

    Hayo yamezungumzwa na kamishina msaidizi mkandamizi wa polisi kikosi cha usalama barabarani kamanda Fortinatus Muslim alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na muendelezo wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mkoa wa dar es salaam ambapo amesema wataadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabara katika mkoa wa kipolisi kinondoni  tarehe 18-25  katika viwanja vya Biafra.

    Aidha kamanda muslim amesema wadhamini wakuu wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani ni stanibic bank ambao wameamua kuungana nao katika juhudi za kupunguza ajali barabarani na kutoa elimu huku akizitaka taasisi nyingine kuungana nao ili kuokoa maisha ya watanzania mbalimbali

    Naye mkuu wa matawi na mitandao wa  stanbic bank bw.Mussa kitoi amesema wao kama stanbic bank wameamua kuungana na kikosi cha usalama barabarani kwani ni swala nyeti na muhimu kwani linamgusa kila mtu hivyo wameandaa video mbalimbali ambazo zitakuwa zinarushwa kupitia luninga mbalimbali ambazo zitakuwa zinatoa elimu kuhusiana na usalama barabarani pia wanaandaa stika maalum ambazo zitakuwa na namba za simu za kikosi cha usalama barabarani ili zitumike kutoa taalifa kama kutakuwa na hatari kwa dereva juu ya maisha ya abiria.

    Naye kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kamanda ameishukuru bank ya stanbic bank kwa kushirikiano wao na amesisitiza kuhusu jukumu la usalama barabarani ni la kila mmoja.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI