Diwani na wananchi wake wamekabidhi vyakula vikiwemo mchele, sembe , mafuta ,sabuni huku mgeni rasmi Mtarawanje amejitolea mabegi ya shule kwa watoto hao.
Diwani uyo amewaeleza vijana hao kuwa elimu ndio msingi wao na ndo mana ameamua kujitokea mabegi ya shule ili wakaweze kutimiza ndoto zao, uku akiwashukuru wananchi wote waliojitokeza kuambatana nae.
Diwani uyo ameiomba jamii kuiga mfano huo na taratibu wa jimbo la Mbagala wa kujitolea kwa wahitaji ambao huanza alfajiri kwa mbio ( jogging).

Akipokea misaada iyo mkuu wa kituo iko Thomas Muhere amewashukuru wote waliojitolea na kuitaka jamii yote kuguswa na kukumbuka watu wenye mahitaji haswa kipindi hiki cha kumaliza Mwaka kama sehemu ya shukrani zao.

Naye Jeniva mlokozi alipata nafasi ya kuwakilisha wasichana hao kwa kutoa shukrani zao za dhati kwa waliojitolea kwa hali na mali kuwakumbuka.
No comments:
Post a Comment