• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 7 December 2017

    Magufuli atinga Dodoma

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo  amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. 
    Katika Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge.
    Akiwa Mkoani Dodoma Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali.
    Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
    Sherehe za Uhuru zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi tarehe 09 Desemba, 2017.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI