Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu
amefunguka na kusema kuwa ameambiwa na madaktari wake kuwa atasimama,
atatembea na kurudi tena Tanzania kuendelea na majukumu yake kama
kawaida.

Aidha Tundu Lissu amesema hajapoteza matumaini ya kuwapata na kuwatambua watu ambao walishambulia kwa risasi kwa kuwa anaamini sehemu ambayo tukio hilo lilitokea kulikuwa na ulinzi na walinzi wa serikali.
"Matumaini hayajapotea kwa vile nakaa kwenye nyumba za serikali hizi nyumba zinalindwa masaa 24, Je, siku hizo napigwa risasi walinzi walikuwa wapi? Walinzi wa geti kubwa nao walikuwa wapi? Ile sehemu yote tunayoishi imezungushwa ukuta na kuna geti kuu lenye ulinzi masaa 24 nao walikuwa wapi? alihoji Tundu Lissu
No comments:
Post a Comment