• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 28 December 2017

     Na Stahmil Mohammed
    Chama cha wafanyakazi Wa sekta ya huduma za mtandao na mawasiliano  Tanzania (TEWUTA) wametoa pongezi Kwa Rais Wa Jamuhuri ya muungano Wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli Kwa kutoa agizo  kuchunguza kampuni ya AIRTEL kama ni Mali ya TTCL.

    Pongezi hizo zimetolewa LEO na Katibu Mkuu Wa chama hiko Bw. Junus Ndaro kwenye mkutano na waandishi Wa habari na kusema kuwa chama hiko kimefurahishwa sana na agizo hilo LA rais na wanamuunga mkono kwani ni suala ambalo walikuwa wakilipigia kelele tangu Mwezi Wa 2 mwaka 2001 kuwa kampuni ya simu ya Tanzania TTCL ilibinafsishwa Kwa Mwekezaji Wa nje ambao ulikuwa na muungano Wa kampuni ya simu ya MSI toka NETHERLANDS na DETECON ya ujerumani na kuunda kampuni ya MSI/DETECON ambapo mwekezaji Huyo alitakiwa kulipa dollars 120 bilioni Kwa ajili ya uwekezaji wake lakini alilipa dolls 60 billioni Kwa makubaliano ya kimkataba kukamilisha malipo yaliyobakia baada ya kukamilishwa Kwa taarifa ya ukaguzi Wa heavy za mwaka 1999 hivyo Kwa mujibu Wa kumbukumbu sahihi wakati wawekezaji hawa wanaingia ubia walikuta tayari TTCL imeanzisha kampuni ya simu ya mkononi Kwa Jina la CELNET Mobile ambayo ilisajiliwa na BRELA na Tume ya Mawasiliano ilikuwa imekwisha ipatia TTCL leseni ya kuanzisha Biashara ya simu za mkononi katika kipindi kifupi baada ya kuingia Wabia kampuni hii ya CELNET ilibadilishwa Jina na kuanzishwa Kwa kampuni ya simu ya CELTEL.

    Aidha Bw.Ndaro ameongeza Kwa kusema kuwa TEWUTA wanaamini kuwa ufisadi uliofanyika kupitia Tamko LA Serikali LA tarehe 30 2005 ambapo katika tangazo hilo lilisainiwa na Ndugu S.H.MSOMA ambaye alikuwa  Katibu Mkuu Wa Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi ambapo serikali ilitoa uamuzi Wa TTCL kumilikiwa Kwa pamoja Kwa hisa 65% na MSI/DETECON(CELTEL) hisa 35% na serikali ya Tanzania  kumiliki hisa 40% katika kampuni ya simu ya CELTEL International hisa 60% Kwa kuzingatia tangazo hilo hivyo Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi iliuaminisha umma Wa Wa Tanzania kuwa CELTEL si kampuni ya TTCL jambo ambalo tulililalamki hadi LEO lakini hatukiwahi kusikilizwa na viongozi husika Kwa kipindi chote hiko jambo ambalo liliwaumiza lakini Kwa sasa wamepata matumaini na faraja makubwa baada ya rais kutoa tamko LA kuchunguzwa Kwa suala hilo .

    Pia TEWUTA imemtaka Waziri Wa fedha kuchunguza suala hilo Kwa umakini kwani ni suala kubwa na lenye Tija Kwa taifa pia TEWUTA imesema IPO tayari kutoa ushirikiano wote kwani wanaushahidi Wa kutosha.

    Kwa upande wake Mwenyekiti Wa chama hiko Bw.Pius Makuke amesema suala hili ni suala lenye Tija Kwa taifa hivyo amewataka Wa Tanzania wote wamuunge mkono rais kwani kampuni ikirudi mikononi mwa mmiliiki halali italeta faida Kwa taifa na ni utambulisho mzuri Wa taifa.
    [12/28, 13:44] Z4news Tv: Z4news tv

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI