Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imekanusha
taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa wanamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu.

“Hizo taarifa sijui zimetoka wapi, lakini sisi hatuna huyo mtu, hatujamkamata saa tunashindwa kuelewa watu wanazusha kwa lengo gani”, amesema Misalaba.

Aidha msemaji huyo ameongeza kuwa wao kama taasisi hawajapokea agizo lolote la kumkamata na kumfanyia uchunguzi ndugu Nehemia Mchechu hivyo hawana sababu ya kumkamata.
Nehemia alisimamishwa kazi na Waziiri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi siku ya Jumamosi wiki iliyopita. Jana jioni kwenye mitandao zilisambaa taarifa za kukamatwa kwake ambavyo leo TAKUKURU imekanusha
No comments:
Post a Comment