• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 22 December 2017

    Tanzania na Uganda zakubaliana

    anzania kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary  Mashingo na Uganda kupitia kwa Balozi wake nchini bwana Richard Tumusiime  Kabonero leo zimesaini makubaliano ya kuboresha sekta ya mifugo.
    Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Bukoba na baada ya kutia saini Dkt. Mary  Mashingo amesisitiza kwamba ushirikiano wa kitaalam katika kuratibu, kufuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini ya kila wakati utaleta mafanikio makubwa  baina ya nchi ya Tanzania na Uganda.
    “Magonjwa ya mlipuko kwa  wanyama  ni suala mtambuka duniani kote, hivyo ni muhimu kulishughulikia  kwa pamoja ili kuwa na tija, pia tumeamua kwa pamoja kuanzia sasa kudhibiti tatizo la utoroshaji wa mifugo kwenye mipaka ya nchi zetu na hatua kali  zitachukuliwa  ili kutoa fundisho kwa yeyote atakayefanya makosa”, amesema Dkt. Mashingo.
    Naye Balozi Kabonero amesema magonjwa ya mlipuko kwa wanyama hayana mipaka hivyo makubaliano yaliyofanyika yatasaidia kudhibiti magonjwa ya wanyama  hatimaye kuboresha  mifugo.
    Kwa upande mwingine Dkt. Mashingo amezitaja  baadhi ya sheria ambazo ni kipaumbele  kwa wafugaji kuzingatia kwa sasa kuwa ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo namba 17 ya mwaka 2003 na  Sheria za Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI