Mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe ambaye ni mdau mkubwa wa michezo
hususani soka amekiombea aunacham wa FIFA chama cha soka cha Zanzibar
ZFA.

Hatua
hiyo imekuja baaada ya timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)
kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge 2017
inayoendelea nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Zitto
amefunguka ya moyoni akitaka ZFA iwe mwanachama wa shirikisho la soka la
kimataifa FIFA pamoja na lile la Africa CAF angalau kwa miaka mitano na
inaweza kupiga hatua ambazo TFF imeshindwa.

“Kama hatutaki Zanzibar kuwa Mwanachama wa FIFA
kama ilivyo Scotland. Tuseme kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu ZFA
ndio mwanachama FIFA na CAF ili TFF ipate muda wa kujipanga. Ndani ya
hiyo miaka 5 nawaambia Zanzibar itakwenda AFCON na hata Kombe la Dunia.
#MsemaKweliMpenziWaMungu”, ameandika Zitto Kabwe.
Zitto ametoa mfano kuwa Zanzibar ingepata uanachama
kamili wa FIFA kama ilivyo kwa nchi za Scotland pamoja na Wales ambazo
pia ni nchi dada za taifa la Uingereza lakini zinatambuliwa na FIFA kama
mataifa wanachama huku Uingereza ikitambulika kama England.
No comments:
Post a Comment