• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 27 January 2018

    CHOZI LA MAKONDA HALITAWAACHA MATAPELI SALAMA




    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kufuatila  mgogoro wao  na kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.
    Nyumba ya wastaafu  inayodaiwa kudhulumiwa na Matapeli.


    Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote. 




    Story ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea mtu anamdhulumu Mali yake.

    Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi. 

    Kwa muda huu  wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba walipewa bure kuishi ,  na msamaria mwema  mmoja aliejitolea  ambapo  Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha na kumuomba aendelee kuwahifadhi hadi hapo mambo yao yatakapo kamilika na kurudi katika nyumbayao. 

    Nao wananchi waliodhurumiwa , nyumba yao wamesema wameridhishwa na hatua alizo chukua mhe. Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa Mungu amejibu maombi yao  na watapata haki yao.

    Pamoja na hayo wazee hao , wamemshukuru mhe.  Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanao dhurumiwa na kuonewa.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI