Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa uongozi wa
kiwanda cha Saruji cha Dangote Mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na
wachimbaji wadogo wa gypsum.

Biteko
ametoa agizo hilo baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na
uongozi ambapo amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha
kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa
wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara
zao.
Aidha Biteko amesema wachimbaji hao wamekuwa wakilalamikia kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao hivyo kuagiza jambo hilo limalizike na watu wapate haki zao.

Katika hatua nyingine Biteko amesema Serikali ya awamu ya tano inalenga kuwasaidia wachimbaji wadogo sambamba na wawekezaji ambao wanapaswa kufanya kazi bila kusumbuliwa.

No comments:
Post a Comment