Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro leo Ijumaa Januari 26,2018 ameungana na wananchi wa
kijiji na kata ya Mwalukwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga (Vijijini) kuziba ukingo wa bwawa la Mwalukwa ambao umebomoka
na kusababisha maji yatoroke.
Matiro aliyekuwa ameambatana na
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bahati Kasinyo Mohammed pamoja na baadhi
watendaji wa halmashauri akiwemo Injinia wa maji Silvester Mpemba
aliungana na wananchi kuziba sehemu ya ukuta/ukingo wa bwawa iliyobomoka
na kusababisha maji yavuje/yatoroke.
Bwawa hilo lililojengwa kwa nguvu ya
wananchi kati ya mwaka 1941- 1951 linahudumia wananchi wa kata ya
Mwalukwa yenye vijiji vinne ambavyo ni Ng’hama,Bulambila,Mwalukwa na
Kadoto B lakini pia kijiji cha Mwamadilanha kilichopo katika kata ya
Pandagichiza.
Akizungumza wa zoezi hilo la kuziba
sehemu ya bwawa inayovuja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
aliwataka wananchi kutunza bwawa hilo wakati serikali inaendelea na
utaratibu wa kufikisha huduma ya maji ya mradi wa Ziwa Victoria katika
vijiji ambavyo havijafikiwa na mradi huo.
“Nimekuja hapa kuungana nanyi
kuongeza nguvu ya kuzuia maji yasitoke,niwapongeze pia kwa kuja,naomba
mtunze bwawa hili kwani kuna maeneo mengine wanatamani kuwa na bwawa
kama hili,maafisa watendaji ,viongozi wa sungusungu na viongozi ngazi za
vijiji na kata wekeni utaratibu wa kutunza hili bwawa kwa ajili ya
matumizi ya binadamu na mifugo yenu”,alisema Matiro.
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga,Bahati Mosinyo Mohamed alisema pesa zilizotengwa
kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo bado hazijafika hivyo kuwataka
wananchi kutokuwa na hofu kuwa huenda pesa zimeliwa na baadhi ya watu.
Nao Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela na katibu wake
Jumanne Katundu walioshiriki katika zoezi hilo,waliwaomba viongozi wa
vijiji na kata kuunda sheria na kanuni kwa ajili ya kutunza bwawa hilo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiangalia maji
yaliyoroka katika bwawa la Mwalukwa lililopo katika kata ya Mwalukwa
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kulia ni wananchi wa kijiji cha
Mwalukwa wakiweka mchanga kwenye mifuko ili kuzuia maji yasitoroke
katika bwawa hilo.
Sehemu ya bwawa la Mwalukwa.
Kulia ni
diwani wa kata ya Mwalukwa Ngassa Mboje akionesha sehemu ambayo bwawa
limemong’onyoka ukuta na kusababisha maji yavuje/yatoroke.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifukia sehemu ya ukingo wa bwawa hilo.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akishirikiana na wananchi
wa kijiji cha Mwalukwa kuchimba udongo kwa ajili kuziba sehemu ya
ukuta/ukingo uliobomoka katika bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akiwa amebeba karai la
udongo aliouchimba kwa ajili ya kuziba ukingo/ukuta wa bwawa la
Mwalukwa.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishirikiana na mwananchi kubeba
mfuko wa udongo kwa ajili ya kuziba ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasititiza wananchi kulinda bwawa hilo
No comments:
Post a Comment