• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 30 January 2018

    Muswada wa sheria wapitishwa bungeni

    Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 5 ya mwaka 2017 zikiwamo mbili kati ya nne zilizopendekezwa ambazo ni sheria ya ardhi, sura 113 na sheria ya utumishi wa umma sura 208.
    Muswada huo umepitishwa leo Bungeni katika mkutano wa 10 wa Bunge kikao cha kwanza mwaka 2018 kilichofanyika mjini Dodoma ambapo kwa sasa ndipo shughuli za kiserikali zinafanyika huko.
    Akisoma muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, amesema muswada huo unapendekeza marekebisho katika sheria ya ardhi sura 113 ambayo katika sehemu ya 10 ya sheria hiyo inaanisha masharti kuhusu kutumia ardhi kupata mkopo.

    Pamoja na hayo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuna marekebisho ya sheria ya utumishi wa umma sura ya 298, ibara ya 12 kuhusu masharti ya umri wa kustaafu kwa kutokuwa na kikomo zaidi ya umri kutajwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa, akitoa maoni ya kamati amesema serikali itengeneze mkakati endelevu kutatua tatizo la madaktari bingwa na wahadhiri wa vyuo vikuu ni uamuzi wenye msingi wa kikatiba katika ibaa ya 13(5) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI