• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 6 January 2018

    Muungano wa VIKOBA kigogo watoa msaada kwa watoto yatima.


    Na Stahmili Mohammed.

    Yatima wanaoishi kata ya kigogo jijini Dar es salaam  leo wamepata neema kutoka kwenye umoja wa vikundi vya kuweka na kukopa hisa vinavyojulikana kwa jina maarufu  la VIKOBA kwa kupewa vifaa vya shule ikiwa ni shuhudi za kuunga mkono Sera ya elimu bure nchini.

    Katika shughuli hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Diwani kata ya kigogo vimeungana vikundi takribani 18 ambapo kwa pamoja wamechanga milioni tatu laki nne na tisini na tano na kununua vifaa mbali mbali kama vile madaftali, kalamu, sare za shule kwa ajili ya kuwagawia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kata ya kigogo.
     
    Akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kutoa msaada kwa watoto wanaokaa mazingira magumu, mwenyekiti kutoka kikundi cha furaha Abdilkareem Mohammed amesema kuwa lengo lao kubwa ni kujikwamua kwenye mazingira magumu na ikiwezekana kusiwepo kabisa na watoto tegemezi.

    "Lengo letu kuu ni kujikwamua kutoka kwenye mazingira magumu na kufuta kabisa uwepo wa watoto tegemezi kwenye jamii yetu" amesema Abdilkareem.

    Aidha katibu kutoka kikundi cha tuamke, Nasma Shabani amesema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira yanayoonekana na yanayoizunguka jamii hivyo itapelekea wao kuondokana na upweke na kujisikia furaha kama watoto wengine wanaoishi mazingira ya kawaida.

    Pia Nasma amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni ugumu wanaoupata pindi wanapowakusanya watoto ili kiwaweka eneo moja Na kuongeza kuwa watoto hao hupatikana kwa njia ya kupita mtaa kwa mtaa na nyumba hadi nyumba.

    "Changamoto tunayokumbana nayo ni kuwakusanya watoto na kuwaweka eneo moja Na tunawapata watoto hawa kwa kutembea nyumba kwa nyumba Na kuzunguka mtaa kwa mtaa" amesema Nasma.

    Kwa upande wake mtoto Abdalah Mussa anayesoma darasa la saba ambaye ni moja ya watoto waliopata msaada Leo amesema kuwa amefurahi kupokea vifaa vipya vya shule na kusema kuwa vitapelekea yeye kufanya kufanya vizuri kwenye masomo yake.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI