Kwa upande Wa sekta ya afya amewaahidi wananchi Wa Kata ya Kigamboni kuwa wanafanya utaratibu wa kufanya vituo vya afya vya umma kutoa huduma bora zaidi na kufikia mwezi ujao katika hospitali ya Kigamboni na vijibweni wataweka x-ray na ultrasound mpya na kwa kituo cha afya kimbiji watakipandisha hadhi Kwa kuweka thieta na milioni 300 itatumika Kwa vifaa.
.

Sambamba na hayo Mbunge huyo amewaahidi wananchi ifikapo mwezi wa pili mwishoni hali ya utulivu wa umeme wa Kigamboni utajirudia na mpaka sasa wanaanza mchakato wa kujenga kutuo cha umeme cha kupooza umeme Kigamboni.

Aidha Kwa upande wa barabara za mitaa zote kuanzia sasa zitasimamiwa na Tarula na siyo halmashauri tena.
Pia amewataka wananchi hao kutumia fursa waliyopewa na meneja wa Bank ya Nmb Kigamboni ya kwenda kuchukua Mikopo na kuwataka wawe waaminifu na kuwa na malengo ya mikopo hiyo watayaochukua.

Mbali na hayo ametoa maagizo Kwa mganga Mkuu wa vituo vya afya Kigamboni kuweka masanduku ya maoni katika vituo vyote vya afya na huduma zote za afya zitangazwe na ziwekwe wazi kwa wananchi na kwa upande wa usalama amewata wahusika wabandike namba za viongozi

No comments:
Post a Comment