Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amefunguka na kumvaa
mwanaharakati Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyo anamchafua na
kutaka kumgombanisha na viongozi wa nchi kwa kusambaza sauti ambayo si
yake.
Ole
Sendeka amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara wa CCM katika
kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge wa jimbo la Longido Arusha kwa
chama hicho na kusema hiyo sauti ambayo inasambazwa na huyo dada
kuonesha kuwa anamzungumzia Rais John Pombe Magufuli vibaya pamoja na
Bunge si sauti yake bali imetengenezwa na watu wa upinzani kwa lengo la
kumchafua na kumchonganisha.
"Akutukanaye hakuchagulii tusi, kupitia mitandao ya kijamii wameendelea kutengeneza na kusambaza 'clip' za kutafuta namna ya kunifarakanisha mimi na viongozi wa Serikali nataka niwaambieni ambazo mmeziona kwenye mitandao zinasambazwa na watu wa upinzani pamoja na sijui Mange Kimambi sijui kitu gani kile, ninaomba mzipuuze kwa kiwango kinachostahili maana zote ni uzushi mtupu" alisisitiza Ole Sendeka.
Katika moja ya sauti ambayo ilikuwa inasambaa ikidaiwa kuwa ni ya Mkuu wa Mkoa huyo wa Njombe ilikuwa inasema kuwa Bunge sasa limeshikwa na kushindwa kufanya kazi yake jambo ambalo limempeleka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mhe. Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha Bunge.

No comments:
Post a Comment