Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali
Mohammed Shein ametunuku nishani zilizotukuka 43 kwa viongozi na
watumishi wa umma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu
ya Zanzibar.

Pamoja na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani .
Katika maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kiuchumi ya taifa hilo.
No comments:
Post a Comment