Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefunguka na kusema
uwezo mkubwa wa Rais Magufuli na Demokrasia ya kweli ni jambo ambalo
linawavutia wageni kuja Tanzania akiwepo Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame
anayetarajiwa kuwasili nchini Jumapili.

Makonda
amesema hayo leo akiwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya
kuagana na Rais Magufuli ambaye ameelekea visiwani Zanzibar kushiriki
sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
"Amani Demokrasia ya kweli, upendo na uwezo wa mkubwa wa Rais Magufuli ndiyo msingi wa kuwavuta wageni kuja kutembelea hakuna mgeni ambaye anaweza kutembelea nchi ambayo haina upendo, amani na mshikamano. Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli inaendelea kuchanja mbuga katika nyanja za kidemokrasia hasa pia katika uwanja mwingine wa kidiplomasia na kuwafanya wageni waone sehemu nzuri ya kuja kutembelea" alisema Makonda
Mbali na hilo Makonda amesema kuwa Rais Paul Kagame atawasili nchini Tanzania siku ya Jumapili ya tarehe 14 ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment