• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 12 January 2018

    Trump akataa kufungua ubalozi mpya wa Marekani Uingereza

















    Rais Donald Trump wa Marekani amefutilia mbali mpango wa kuzuru nchini Uingereza mnamo mwezi Februari ambapo alikuwa ametarajiwa kufungua ubalozi mpya wa taifa hilo uliogharimu takriban dola bilioni moja.

    Katika ujumbe wake kwa Twitter, rais huyo wa Marekani alisema yeye sio shabiki wa ubalozi huo mpya ambao unahamia kutoka Mayfair kuelekea mjini London akidai kuwa ulikuwa ''mpango mbaya''.
    ''Jumba la zamani la ubalozi huo liliuzwa kwa fedha chache na utawala wa rais Obama'', aliongezea.
    Downing Street ilikataa kutoa tamko kuhusu hatua hiyo ya rais Trump.
    Muhariri wa BBC kaskazini mwa Marekani Jon Sopel alisema kuwa kuna uwezekano wa maandamano katika barabara za mji wa London iwapo angezuru.
    Hatua hiyo ya ubalozi wa Marekani ilithibitishwa mnamo mwezi Oktoba 2008 wakati rais George W Bush alipokuwa mamlakani.




    Ujumbe wa rais Trump aliouweka katika mtandao wa twitterHaki miliki ya pichaTWITTER
    Image captionUjumbe wa rais Trump aliouweka katika mtandao wa twitter

    Hatahivyo rais Trump aliulaumu utawala wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama kwa kuuza eneo zuri la ubalozi huo kwa ''fedha chache''.
    Alisema kuwa jengo hilo jipya katika eneo la Vauxhall, kusini mwa London lilikuwa katika eneo baya, akiongezea.''Walitaka mimi nilifungue rasmi-Hapana!''.

    chanzo BBC Swahili

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI