Wanamitindo wa Tanzania wameungana na kuanzisha chama chao ili kuendeleza na kukuza maslahi ya sekta ya mitindo nchini.
Chama
hiko cha mitindo kitakachojulikana kama Fashion Association Tanzania
kinalengo la kuendeleza maslahi ya sekta ya mitindo kwa kuwaunganisha
ili kugawana ujuzi,uzoefu na rasilimali za sekta hiyo ya mitindo nchini.
Hayo
yamesemwa Na Mwanzilishi wa chama cha mitindo Tanzania Mustafa
Hassanali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
chama hiko amesema chama hiko kimeanzishwa kuwa chenye nguvu na taaluma
ya uwezo wa kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini pia kuunga
mkono juhudi za rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.john pombe
Magufuli katika kuifanya nchi yetu kuwa katika uchumi wa kati wa
Viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kwa
upande wake Rais wa shirikisho la sanaa nchini Adrian Nyangamalla
amewapongeza wabunifu kwa hatua nzuri walioichukua kwani kimekuja
wakati muafaka ambapo wasanii mbalimbali wanatakiwa kujisajili kwa
makundi wawe wananufaika kupitia na wawe wanachangia uchumi wa nchi.
Naye
Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza amesema hatua iliyofikiwa
na wanamitindo itasaidia wasanii kuwa katika utawala bora hivyo ni jambo
la kuungwa mkono na Basata itashirikiana hayo began kwa began
kuhakikisha chama hiko kinapiga hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment