Na Stahmil mohamed
Wanawake
wametakiwa kujiamini,kuongeza ubunifu katika biashara zao ili kufikia
malengo mbalimbali waliyojiwekea Na kwa Taifa kiujumla.
Hayo
yamesemwa Na mkurugenzi wa IPP media Regional Mengi alipokuwa
akizungumza na chama cha wanawake wafanyabiashara Na
wajasiliamali(TWCC)waliokutana katika semina ili kujadili masuala
mbalimbali kuhusiana na chama chao pia kuboresha bidhaa zao ili kufikia
malengo waliyojiwekea ambapo amewataka wanawake kuwa Na macho ya kuona
fursa ili kuzidi kujiingizia kipato ,kujiamini,kuendana Na Na
teknologia.
Aidha
Mengi amewaonya wanawake kuwa kuwataka waache majivuno badala yake wawe
wanyenyekevu ili kuongeza wigo wa kukuza biashara Na amehitimisha kwa
kuwakabidhi jengo kwaajili ya kufanyia shughuli zao pamoja Na
kujifunzia shughuli mbalimbali.
Naye
mkurugenzi wa uwezeshaji Baraza LA Taifa LA wananchi kiuchumi bi.Anna
Dominic amesema Baraza litaanza kutoa mikopo kupitia saccoss
walioianzisha
Naye
mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Na
wajasiliamali(TWCC)bi.Jacline Mnenea amemshukuru Mengi kwa kuwakabidhi
jengo hilo kwaajili ya kufanyia shughuli zao pamoja Na mafunzo
mbalimbali kwani kutawasaidia kufanyia Nazi zao kwa weledi.
|
No comments:
Post a Comment