Waziri wa maliasili na utali Khamisi Kigwangala amewataka
watendaji wa wizara ya maliasili na utalii kushirikiana kwa pamoja ili
kuhakikisha sekta ya utalii inakua nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa
kamati ya kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi za mwezi maalum wa
maadhimisho ya urithi wa taifa la Tanzania amesema sekta ya uatalii imekuwa na
mchango mkubwa katika kuchangia pato la
taifa kukua.
Sambamba na hayo Mhe.Kigwangala amesema mpaka sasa sekta ya
utalii imekuwa imejikita zaidi katika utalii wa wanyama pori ili kuwavutia
watalii wanaongia nchini kwa wengi wao wanavutiwa zaidi kuangalia wanyama pori.
Aidha ameitaka kamati hiyo inayoandaa maadhimisho hayo wahakikishe
wanaandaa mpango maalum wa kuelimisha jamii juu ya mila na tamaduni zao za
kitanzania na kutangaza lugha ya taifa (Kiswahili) nje ya nchi.
Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo amesema wao kama kamati wanakazi kubwa ya kutumia maadhimisho hayo kuweka
mikakati ya kuongeza utalii wa ndani kwani bado watanzania wengi hawana
utamaduni wa kutembelea mbuga zetu na vivutio vya ndani

No comments:
Post a Comment