• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 13 January 2018

    Wizara ya Nishati yatakiwa kujitathmini

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati ijiridhishe na ubora wa vifaa vinavyotumiwa na wakandarasi katika miradi ya umeme.
    Ametoa kauli hiyo leo  wakati akizungumza katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika , Ofisini kwake, Dodoma ambapo ametaka  iwasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya miradi inayotekelezwa inalingana na kiasi cha fedha wanacholipwa wakandarasi hao.
    Waziri Mkuu amesema wakati huu ambao Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiendelea na miradi ya usambazaji umeme, na kuongeza kwamba  ni vema wizara hiyo ikajiridhisha na ubora wa vifaa.
    “Wasimamieni wakandarasi kikamilifu na kama hamjaridhishwa na kazi wanayofanya msisite kuwachukulia hatua, tunataka  wananchi wapate umeme.” Majaliwa
    Amesema Rais Dkt. John Magufuli amedhamiria kuona umeme unasambazwa kwenye vijiji vyote nchini kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.
    Waziri Mkuu amesisiza kwamba ni lazima wakandarasi waliopewa jukumu hilo wasimamiwe kikamilifu ili mradi hiyo iweze kuwa na ubora unaostahili.
    Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dkt.  Medard Kalemani amesema tayari wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA namba tatu wameshaanza kazi.
    Amesema kwa wakandarasi ambao bado hawajaanza wamekubaliana kwamba wataanza wakati wowote na wa mwisho utaanza Machi 2, 2018 na kuongeza kwamba  wizara yake itahakikisha miradi yote ya kusambaza umeme inasimamiwa kikamilifu na inakamilika kwa wakati na katika ubora unaostahili. CHANZO EATV

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI