• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 2 February 2018

    IGP Sirro atoa tamko kwa jamii

    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameitaka jamii pamoja viongozi wa dini kushirikiana na Polisi ili kutokomeza makosa mbalimbali katika jamii ikiwemo, mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi, ulevi, ubakaji ili kuiweka nchi salama zaidi.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Simon Sirro.
    IGP Sirro ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa takwimu za sasa zinaonyesha matukio ya aina hiyo yamekithiri sana nchini Tanzania jambo ambalo jamii inapaswa kubadilika ili kupunguza matukio hayo.
    "Kuna makosa ambayo watu lazima wabadilike na hili haliitaji Jeshi la Polisi maana mimi nasimamia  Sheria lakini kuna viongozi wa dini wazungumzie hayo mambo. Muumini wako akija Kanisani au Msikiti na ukimwambia katazo la Mungu anaweza akabadilika", alisema IGP Sirro.
    Kwa upande mwingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Sirro amesema kuna makosa ambayo viongozi wa dini wakishiriki kwa ukaribu zaidi inaweza kupunguza huku akiitaka jamii kubadilika kitabia ikiwemo kuachana na ulevi wa kupindukia.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI