• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 23 March 2018

    ALMUNTAZIR WAITAKA JAMII KUWAPELEKA SHULE WATOTO WENYE USONJI

    Ikiwa Leo ni Siku ya Kimataifa ya Daunsyndrome duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo March 21 kila mwaka,Jamii imetakiwa kutambua kuwa elimu ni haki kwa Watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo watoto wenye matatizo ya Dounsyndome, ikiwemo Usonji.


     Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Makamu Mkuu wa Shule ya wasichana ya Almuntanzil yenye kitengo cha msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu -AMSEN- Joan Soka alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo wenye Usonji,Utindio wa Ubongo na Dounsyndrome na kuwakosesha elimu jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Sekikali.
     Kwa upande wake Mtaalamu wa elimu maalumu kwa watoto hao kutoka AMSEN Nyembezi Mbano amesema utafiti unaonyesha watoto hao wakifundishwa kwa kufuata kanuni sahihi watoto hao wanauwezo wa kuelewa na kushiriki katika shughuli mbalinmbali za kijamii ikiwemo ufundi stadi.



    Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Almuntanzil Mahmood Ladak amesema Taasisi hiyo kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu mwaka 2013 iliamua kuanzisha kitengo hicho cha msaada kwa watoto hao ili kuwasaidia watoto hao na kuunga mkona mkakati wa Serikali wa kutaka watoto wote wapate elimu na kueleza kuwa wamezingati umuhimu na umaalumu  wa watoto hao na hivyo wanavifa vya kufundishia ambavyo vinawafanya kuelewa na kupenda kujifunza.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI